Psalms 105:28-33


28 aAlituma giza na nchi ikajaa giza,
kwani si walikuwa wameyaasi maneno yake?

29 bAligeuza maji yao kuwa damu,
ikasababisha samaki wao kufa.

30 cNchi yao ilijaa vyura tele, ambao waliingia
hadi kwenye vyumba vya kulala vya watawala wao.

31 dAlisema, yakaja makundi ya mainzi,
na viroboto katika nchi yao yote.

32 eAlibadilisha mvua yao ikawa mvua ya mawe,
yenye umeme wa radi nchini yao yote,

33 fakaharibu mizabibu yao na miti ya tini,
na akaangamiza miti ya nchi yao.
Copyright information for SwhKC